Halmashauri ya mji Newala imeidhinishiwa bajeti ya shilingi bilioni 16.3 na bunge la bajeti lililoishia Juni 2019 kwa ajili ya kukusanja na kutumia ili kutekeleza bajeti yake ya maendeleo ya mwaka 2019/2020.
Hayo yameelezwa jana Juni 19,2019 na Afisa mipango wa halamashari hiyo Bi. Sophia Makungu wakati anasoma taarifa ya bajeti idhinishwa ya halmashauri hiyo kwa mwaka fedha 2019/2020 kwenye mkutano wa baraza la madiwani wa robo ya nne 2018/2019
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Ndg. Andrew Mgaya amesema ili bajeti hiyo iweze kufikia malengo kusudiwa ni lazima kuwe na ushirikianao katika kuisimamia hasa katika kukusanya mapato ya ndani kupitia tozo zilizopo kisheria.
Aidha amewasisitiza waheshimiwa madiwani kuwa mstari wa mbele kuwahamasisha wananchi kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye maeneo yao, na jambo hilo likifanyika kwa ukamilifu utekelezaji wa bajeti hiyo utafikia asilimia 100.
Naye Mwenyekiti wa halmashuri hiyo Mhe. Sambili Mohamedi amesema ili kufikia malengo ya bajeti hiyo kuelekea msimu mpya wa korosho 2019/2020 ni lazima kuwe na usimamisimu madhubuti wa kuziba mianya ya utoroshaji korosho kwenda halmashauri nyingine au uuzaji kwa njia ya kangomba.
Hata hivyo amezitaja Kata za Mkunya, Mcholi1, Mcholi2 na Nanguruwe kuwa ni maeneo ambayo yana njia nyingi za kutorosha korosho hivyo amewataka Maafisa watendaji kuwa makini pamoja na madiwani kutowatetea wananchi wao pale wanapokamatwa na makosa kwani kufanya hiyo ni kuikosesha halmashauri mapato.
Kwa upande mwingine ametoa pongezi kwa Mkurugenzi wa halmasshauri kwa kuchaguliwa na baraza la ushauri la Mwa Mtwara kuwa mkurugenzi bora kati ya wakurugenzi wote 9 wa mkoa huo kwa kuisimamia vizuri halmashauri yake kwenye matumizi bora ya fedha na kutekeleza miradi ya maendeleo kikamilifu.
Picha
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa