Taasisi na vitengo vinavyosimamia usafi wa mazingira halamshauri ya Mji Newala, zimetakiwa kushirikiana kutoa elimu wa uhifadhi mazingira na utunzaji wa miundo mbinu ya barabara kwa wananchi.
Agizo hilo limetolewa na mwenyekiti wa mkutano wa baraza la madiwani ambaye pia ni Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Newala Ndg. Geofrey Nnauye katika kikao cha robo ya nne 2024/2025.
“Tuelimishe umma tupite kwenye mitaa na P.A ili tutoe elimu juu ya uhifadhi wa barabara, masuala ya usafi wa mazingira ni kujukumu la kila mwananchi kufahamu umuhimu wake ikiwezekana tutumie na sheria”.
Nnauye amesisistiza kuwa serikali inaleta fedha nyingi kutekeleza miradi ya Barabara hata sasa zipo barabara za mitaa 11 zinazoenda kujengwa kwa kiwango cha kimataifa hivyo lazima wananchi wapewe elimu ili wazitunze.
Mwenyekiti huyo ametoa agizo hilo kufuatia changamoto iliyowasilishwa na meneje wa wakala wa barabara vijijini na mijini (TARURA) wilayani Newala Mwandisi Sylvester Balama ambaye alieleza wananchi wanachoma taka wenye mitaro ya barabara na kuchoto mchanga katikati ya barabara za udongo.
“Changamoto kubwa wananchi kutupa taka na kuzichoma moto zikiwa kwenye mitaro, mitaro ile imejengwa kwa mawe na saruji kwahiyo ukichoma moto ni wazi kuta zitapasuka”
Hata hivyo Mwandisi Balama ameeleeza katika robo ya nne serikali imewapatia kiasi cha shilingi milioni 190 kwa ajili ya kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo na mradi wa barabara ya Kiuta-Mkunya pamoja na barabara ya Chitandi.
Kwa upande katibu tawala wa wilaya ya Newala Ndg. Thomas Safari amesisitiza kuwa jukumu la kudhibiti uharibifu wa mazingira ninapaswa kusimamiwa na taasisi, wadau na jamii yote ili kuepuka athari zaidi.
Halmashauri ya Mji Newala imefanya mkutano wa baraza la madiwani chini ya Mkurugenzi na kamati ya wataalam (CMT) kutokana na kuvunjwa kwa baraza la madiwani waliochaguliwa na wananchi kwa mujibu wa sheria baada ya kufika ukomo wake.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa