Wakazi wa Kijiji cha Msilili Kata ya Mcholi II Halmashauri ya Mji Newala mkoani Mtwara wameishukuru Serikali kupitia mradi wa Mpango wa kunusuru Kaya Maskini Nchini (TASAF) kwa kutekelezea mradi wa zahanati katika kijiji chao umbao utawanufaisha watu 6,000.
Wakazi hao wametoa shukrani hizo Jumanne 18/07/2023 kijiji hapo wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Kazi Maalum na Mbunge wa jimbo la Newala Mjini Mhe. George Mkuchika ya kuongea na wananchi kuhusu maendeleo yanayofanywa na serikali pamoja na jimbo.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Ndg. Abdulazizi Chapacha amemwambia Mhe. Waziri kuwa wanaishukuru serikali kupitia TASAF kwa kuliona hitaji lao la mda mrefu na kutoa fedha shilingi milioni 101 kutekeleza mradi huo ambao ni mkombozi kwa wananchi wa Msilili kwa huduma za afya.
Mwenyekiti huyo amesema wananchi kwa nguvu zao waliwahi kujaribu kujenga zahanati kwa nguvu zao lakini wahakuweza, “tuliwahi kujaribu kujenga kwa nguvu zetu lakini hatukufika pote, kwakwli tunaishukuru serika tunamshukuru Rais wetu Samia pamoja na TASAF, sisi wananchi tupo pamoja na Serikali ya Mama Samia”. Alieleza Ndg. Chapacha.
Kwa uapande Waziri Mkuchika amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo anawatumikia watanzania na wananchi huku akiwaomba wananewala kuendelea kumuunga mkono mheshimiwa Rais ili wazidi kuona matunda ya awamu ya utumishi wake.
Bi. Sophia Mkatenda mkazi wa kijini hapo amesema TASAF imekua kama mkombozi kijiji kwao kwa kuwa walikua wanatembea kilometa 8 kufuata huduma za afya hali ambayo alikua ni Changamoto hasa kwa wanawake wajawazito.
Bw. Mustafa Chilumba mjumbe wa serikali ya kijiji ametoa pongezi kwa mbunge wao kwa uwakilishi wake wa kutoa msukumo wa kupata miradi ya maendeleo katika jimbo lake. “kwanza tunaishukuru serikali na haya yote yanafanyika kutokana na kuwa na mbunge anaetusemea vizuri, tunamshukuru mbunge wetu”. Alisema kiongozi huyo.
Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Mji Newala Ndg. Alphayo Zakaria amesema mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Msilili umetokana na uhitaji wa wananchi wenyewe ambao waliibua wakati wa mapendekezo na TASAF iliona ni mradi sahihi sambamba na mradi wa kisima unaotarajiwa kutekelezwa kwa wastani wa shilingi milioni mbili.
Zakaria amepongeza mwitikio wa wanamsilili ambao amesema wametoa ushirikiano wa asilimia 100 katika utekelezaji wamejitoa kikamilifu na kuleta maana halisi ya ushiriki wa jamii katika shughuli za maendeleo huku akibainisha kuwa ujenzi wa zahanati hiyo upo kwenye hatua ya umaliziaji.
“Wananchi mradi huu wameutekeleza kwa kujitosheleza, wamejitoa kwa asilimia zote, kile ambacho wametakiwa wajitolee wameonyesha mchango ambao ni nguvu za jamii kwa kiwango kinachotakiwa kinachorisha nakupitiliza hari walio ionesha wasiiache.” Alieleza Zakaria
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa