Wahitimu wa stashada katika chuo cha Uuguzi na Ukunga Newala, wametakiwa kuzingatia maadili ya kazi wawapo kazini na kujiepusha na vitendo vya rushwa.
Rai hiyo imetolewa na mgeni rasmi wa mahafali ya wahitimu 67 mwaka 2025, Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Newala Ndg. Geofrey Nnauye akimuwakilisha Mkuu wa wilaya Newala Mhe. Mwangi Kundya.
Aidhq Ndg. Nnauye amewahimiza uadilifu kazini pale wanapokuwa katika ajira “mnapokuwa kazini jiepusheni sana ujanja ujanja zingatieni maadili ya kazi msipende fedha jiepusheni na rushwa”
Kwa upande wake Jaji wa Mahakama kuu kanda ya Mtwara Mhe. Martha Mpaze amewahasa wahitimu hao kwenda kuwahudumia wananchi bila kuwabagua kwa kuwa kazi yao inahitaji upendo na huruma.
“Huduma yenu ni ya huruma sana, bebeni moyo wa huruma, bebeni moyo wa upendo, mkaokoe maisha ya wananchi bila kuwabagua kwa hali hazo za kiuchumi au wadhifa wao” Amewasisitiza
Hata hivyo Mkuu wa chuo hicho Bi. Gloriana Ngole amesema wanaamini wahitimu hao watakuwa mabalozi wazuri kwakuwa wameonesha nidhani inayofaa pamoja na matokeo mazuri kwa muda wote waliokaa chuoni.
Ngole amesema “Nendeni mkaendeleze nidhamu yenu mliyonayo hata mtakapokuwa kazini, mmekuwa na ufaulu pamoja na nidhani ya hali juu makawe mabalozi wa kukitangaza chuo chetu vizuri”
Chuo cha Uuguzi na Ukunga Newala moja ya vyuo vikongwe nchini ambacho kilianzishwa mwaka 1996 kikiwa kinatoa mafunzo ya uuguzi pamoja na ukunga kwa ngazi ya stashada.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa