Mganga Mkuu wa Halamshauri ya Mji Newala Dkt. Joseph Fwoma amesema jumla ya wananchi 558 wa Halmashauri ya mji Newala wamejitokeza kupatiwa chanjo ya UVIKO-19 katika tamasha la kampeni ya uhamasishaji chanjo ilipewa jina la Mziki Mnene na kuwataka wengine kujitokeza kuchanja kwa hiari.
Dkt. Fwoma ameyabainisha hayo leo Ijumaa 29/07/2022 ofisini kwake baada ya kuhitimisha kampeni hiyo ilifanyika jana kata za Mkoma 1, Makonga, Namiyonga, Lidumbe na kuhitimishwa viwanja vya kituo kikuu cha mabasi Newala mjini.
Amesema chanjo ya UVIKO-19 ni kinga dhidi ya ugonjwa wa Korona ambao ni hatari na kusababisha kifo kwa haraka na kampeni hivyo ilikua ya kuhamasisha lakini zoezi la kutoa chanjo ni endelevu katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya pamoja na huduma inayotembea kupitia Mkoba hivyo kila mmoja anapaswa kujilinda mwenyewe na kumlinda na mwenzake kwa kupata chanjo.
Hata hivyo amefafanua kuwa chanjo hiyo haina madhara yoyote kiafya kinyume na baadhi ya mitazamo ya watu wakihusisha madhara ya upungufu wa nguvu za kiume au chanjo inayolenga kuchukua takwimu za mambo yanayohusiana zombi haina ukweli na imelenga mitazamo hivyo imelenga kupotosha umma.
Dkt. Fwoma amesema chanjo ya UVIKO-19 imethibitishwa mashirika ya ubora wa dawa ya kimataifa na Serikali kupitia wizara ya afya isingeweza kuidhinisha kutumika kama ingekua na madhara kwa wananchi wake.
Fwoma amefafanua kwa kusema “nawaambia tu watu waje wakachanje kulikuwa na watu wengi wana dhana potofu.. offcourse nyingine zilikua zinazushwa kwamba chanjo ni mbaya, chanjo sijui ina madhara, chanjo inasababisha damu kuganda na nini na vitu kama hivyo, sijui chanjo inapunguza nguvu za kiume na vitu kama hivyo hizi nanii zote hazina ukweli wowote na issue ya kuganda damu mpaka utafiti umefanyika wenzutu wamefanya utafiti wakagundua hizi roumase sio za kweli”.
Mchanganuo kwa waliojitokeza kuchanja ndani ya Halmashauri ya Newala ni Kijiji cha Mkoma 1 waliopata chanjo ni 42 wanaume 13 na wanawake 29, Kijiji cha Makonga watu 33 wanaume 10 na wanawake 23, Kijiji cha Namiyonga watu 59 wanaume 42 na wanawake 17, Kijiji cha Lidumbe watu 30 wanaume 8 na wanawake 22, Stendi ya mabasi Newala mjini watu waliojitokeza 422 wanaume 122 na wanawake 300.
Tamasha la kampeni ya chanjo ya UVIKO-19 lililopewa jina la Mziki Mnene chini ya kauli mbiu Ujanja Ni Kuchanja ndani ya Halmashauri ya mji Newala lilifanyika jana Alhamisi 28/07/2022 likijumuisha burudani ya muziki kutoka wasanii maarufu nchini na waigizaji kama Wema Sepetu, Man Fongo, Mkojani na wengine wengi.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa