Wananchi wa Halmshauri ya Mji Newala wametakiwa kuchukua tahadhari za kujikinga na maambukizi ya magonjwa ya mlipuko kufuatia kuenea kwa ugonjwa wa kichocho katika vijiji vya kata ya Mcholi I, Mcholi II na Mtumachi.
Rai hiyo imetolewa Machi 30, 2023 na Mkuu wa Wilaya ya Newala Mhe. Mwangi Rajabu Kundya kwenye kikao maalum cha kamati ya Afya ya Msingi kilichoketi kujadili mlipuko huo uliojitokeza hivi karibuni.
Mhe. Kundya amewataka wananchi kuchukua tahadhari ya ugonjwa huo wakati taratibu za utoaji wa chanjo zikiendelea kwa kuwa madhara yake ni makubwa kiafya na uchumi.
“Ugonjwa huu ni hatari na unaathiri sio tu kwa afya pekeyake hata uchumi wa eneo husika unaathiriwa, hivyo tunawaomba wananchi wachukue tahadhari za kujikinga na maambukizi wakati taratibu za utoaji wa chanjo kwa wananchi wote zikifuatiliwa”Alifafanua Kundya
Hata hivyo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Yusuph Kateule amewaomba viongozi wa vijiji, kushirikiana na viongozi wa dini katika maeneo yao kuongea na wananchi juu ya madhara ya ugonjwa wa kichocho na kuwashirikisha wataalamu wa afya katika utoaji elimu hasa juu ya umuhimu chanjo zinazotolewa.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Hospital ya Halmashauri ya Newala Dkt. Ramadhani Shabani amewasisitiza wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya mlipuko huo huku akieleza madhara yake kuwa ni makubwa ikiwemo kuvimba tumbo, figo kuharibika, saratani ya kibofu, matatizo ya moyo, kushindwa kufanya kazi pamoja na kifo.
Aidha imeelezwa kuwa rahisi kupata maradhi hasa katika kipindi hiki cha mvua kwa kuwa vimelea uenea kwa njia ya mkojo au maji yaliyochanyika na mkojo wa muathirika hivyo ni wakati wa kutunza mazingira yawe safi, kwa kukata nyasi na kufukia vidimbwi vya maji vinavyoweza kusababisha kuzaliana kwa vimelea vya kichocho.
Akiongea wakati anafunga kikao hicho Mkuu wa Wilaya amewataka viongozi wa kata na vijiji na wananchi kwa ujumla kujianda kupokea chanjo za ugonjwa huo siku chache tu baada ya kumaliza mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa