Wananchi wa jimbo la Newala mjini wametakiwa kutambua kuwa serikali imeadhamiria kuleta maendeleo ya kweli hivyo wananchi wajitoe kikamilifu wakati wa utekeleza miradi ya maendeleo.
Hayo yameelezwa leo na 3/12/2021 na Mbunge wa jimbo hilo Mhe. George Mkuchika ambaye pia ni Waziri Ofisi ya Rais Kazi Maalum wakati wa ziara yake ya kuongea na wananchi kwa njia mikutano ambapo amesema serikali imeshatoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya barabara, elimu na Afya.
“Sisi kwa sasa tupo mjini kwa maana ya halamshauri ya Mji, pamoja na kuwa tulifanya vizuri tukiwa kama wilaya lakini kwasasa mji wetu umezidi kuwa na hadhi ya mji, barabara za lami zimeongezeka, kuna mataa ya brabarani, tumepata kituo cha afya Mkunya, High school mbili za wasichana Kiuta na Nangwanda, Zahanati 11 na nyumba za waganga na hayo ni baadhi tu” amefafanua Mhe. Mkuchika.
Mhe. Mkuchika amesema tayari halmashauri ya Mji Newala imepokea shilingi milioni 470 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari Makondeko Kata ya Makote, Shilingi milioni 250 kwa ajili ya ujenzi kituo cha Afya Mnekachi, pamoja na hamashauri ya mji Newala kuingizwa kwenye mradi wa miji 9 inayofadhiliwa na Benki ya Dunia katika ujenzi wa Barabara, Mifereji na Madaraja.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmshauri ya Mji Newala Mhe. Yusuph Kateule umewataka wananchi kusimamia suala la ulinzi na usalama kwa kuwa maendeleo yanafikiwa kirahisi pale panapokuwa na amani nautulivu hivyo ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha Newala inabaki salama ukizingatia halamshauri hiyo ipo mpakani na Nchi ya Msumbiji ambako hali ya usalama si shwari.
Mhe. Kateule amesema “hali ya usalama kwa ndugu zetu Mozambique tunajua sii shwari na wakati mwingine hata ndugu zetu wengine wapo huko, tunapoona wamerudi tuwaripoti ili wachunguzwe na vyombo vya usalama kama hawana tatizo tuendelee kushirikiana nao na yule atakaeonekana hayupo salama hatua zichukuliwe, amani yetu ikipotea maendeleo hatuna wala utulivu hakuna” ameeleza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapindizi wilayani Newala Ndg. Jabiri Mtanda amesema wananchi waendelee kuwaunga mkono viongozi waliowachagua kwa lengo la kuharakisha maendeleo na kufikia malengo kama ilani ya chama ilivyoainisha.
Katika ziara yake ya siku ya pili ameongea na wananchi wa Kata za Tupendane, Namiyonga na Makote.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa