Wananchi, watumishi wa umma, wadau wamaendeleo pamoja na Madiwani wa halmashauri ya mji Newala kwa pamoja wametakiwa kushikamana katika kusimamia na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa ndani ya halamshauri hiyo.
Rai hiyo imetolewa Leo Ijumaa Januari 31, 2020 wakati wa mkutano wa siku ya pili wa baraza la madiwani wa robo ya pili 2019/2020 na mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mhe. Sambili Mohamedi ambapo ameeleza kuwa umefika wakati wa kila mmoja kutumika pasipo kuangalia changamoto za kiutendaji zilizopo ili kufikia malengo kusudiwa ya maendeleo.
Aidha amewataka watendaji wa kata kuawalika maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwenye mikutano yao ya vijiji na kata ili wananchi wapewe elimu juu ya athari za rushwa na njia za kutoa taarifa za matukio ya rushwa yananyojitokeza katika maeneo yao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya hiyo Ndg. Andrew Mgaya amewata wananchi kuudhuria vikao mbalimbali ili kufikia makubaliano ya kutekeleza shughuli za maendeleo katika maeneo yao na kuondokana na dhana kuwa shughuli hizo hawazifahamu.
Aidha Mkurugenzi amesema lipo tatizo la wananchi kugomea kuchangia michango iliyokubaliwa katika vikao kutokana na baadhi yao kutoshiriki mikutano hiyo na unapofika wakati wa utaekelezaji, hulalamika kuwa hawajui lolote hivyo ni muhimu kubadili fikra ili wananchi wote washiriki kuleta maendeleo yao.
Katika kipindi cha robo ya pili Oktoba - Disemba 2019/2020 halmashauri ya Mji Newala imetumia shilingi bilioni 4.5 kutekeleza shughuli zake pamoja na miradi mbalimbali ya maendeleo.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa