Katika kuadhimisha awamu ya pili ya mwezi wa siku ya afya na lishe ya mtoto Juni 2025, halmashauri ya Mji Newala, wanaume wametakiwa kukijitokeza kushiriki katika masuala ya afya na lishe ili jamii iwe na malezi mazuri sambamba na kuimarisha matokeo bora ya ukuaji wa watoto.
Hayo yameelezwa na Bw. Mwistala Lazima kutoka kijiji cha Kazamoyo kata ya Mnekachi katika halamshauri hiyo ambaye ameeleza kuwa wanaume kujitokeza katika siku za maadhimisho ya lishe ni njia mojawapo ya kuimarisha malezi ya familia.
“Mimi kama mzazi inanilazimu niwe na upendo kwa familia yangu hivyo niwasisitize wanaume wenzangu wawe wanashiriki kwenye haya mazoezi yaani wasiwe wazembe hii inaweza ikasaidia pia kuwa walezi bora kwenye familia zao”.
Aidha Bw. Lazima amefafanua kuwa anatambua ukuaji nzuri wa mtoto unatokana na upatikanaji wa lishe bora na hiyo ndio sababu ya yeye kujitokeza mara zote yanapofanyika maadhimisho hayo kwa lengo la kupata elimu itayoisaidia familia yake.
Naye Bi. Ashura Mnipela mmoja wa wanawake waliodhuria siku hiyo amewaomba wamama kuwa mstari wa mbele katika kuhamasika na kuzingatia masuala ya afya na lishe ya mtoto kwa kuwa inasaidia kuimarisha ukuaji.
“Mimi nimeona watoto walikua awaongezeki kwa kilo sasa angalau ninapojifunza mambo ya lishe na jinsi ya kupika angalau wanaongezeka uzito pia, lakini pia nawahamasisha na wanawake wenzangu wengine hapa hawapo wapo mashambani wasiwe na moyo huo, tuendelee kuambatana na hamasa hizi za lishe”.
Kwa upande wake Afisa lishe wa halmashauri ya Mji Newala Bi. Beatrice Saria amebainisha kuwa maadhimisho ya mwezi wa siku ya afya na lishe ya mtoto yanawahusisha watoto wa chini ya miaka mitano na yanafanyika mara mbili kwa mwaka, mwezi wa sita na mwezi wa kumi nambili.
Hata hivyo Bi. Saria ameeleza kuwa katika awamu hii wamezifikia kata zote 16 kutoa matone ya vitamini A, kutoa dawa za minyoo ya tumbo, kufanya tathmini ya hali ya lishe, mapishi darasa pamoja na kutoa elimu ya ulaji sahihi kwa kuzingatia makundi sita ya chakula.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa