Wanawake wametakiwa kudai na kuzifikia haki zao kwa njia sahihi huku wakijiamini katika utendaji wao na kuachana na dhana pamoja na mitazamo ya kupewa kipaumbele kutokana na jinsi yao.
Hayo yameelezwa leo Ijumaa Machi 04, 2022 na mgeni rasmi Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji Newala Mhe. Yusuph Kateule wakati anafunga mdahalo wa kujadili kaulimbiu ya maadhimisho ya siku ya mwanamke duniaiani “Kizazi Cha Haki Na Usawa Kwa Maendeleo Endelevu”, uliofanyika ukumbi wa mikutano wa halamshauri ya Mji Newala.
Mhe Kateule amesema wanawake wengi wamekua na tabia ya kutaka kuonewa huruma au kupitia njia haraka ili kupata mafanikio kitu ambacho kinaondoa maana halisi ya harakati zao na kujenga taswira ya kuwa bado wanahitaji kuwezeshwa dhana ambayo kwa sasa ni potofu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Newala Bi. Shamim Mwariko amewataka wanawake kutambua umuhimu wa mwanamke kuchukua hatua yakubadili mtazamo kwa lengo la kuliinua Taifa kutokana na nguvu aliyonayo mwanamke.
Afisa Tarafa ya Newala Bi. Mary Twamgabo amesema wanawake wanatakiwa kushikamana na kuwa mabalozi wa kuwapa elimu ya kuitambua haki yao wanawake wengine ili kulifikia lengo kuu la kupata haki na usawa katika jamii.
Mkurugenzi wa taasisi ya utetezi wa wanawake na watoto Newala (NEWNGONET) Bi. Halima Nambunga amesema kwasasa malengo ya wanawake si kutafuta kuwezeshwa au upendeleo bali ni kuona namna ya kupata nafasi sawa katika Nyanja na maeneo ambayo bado hayana usawa wa kijinsia.
Maadhimisho ya siku ya mwanamke ulimwenguni yanafanyika kila mwaka ifikipo Machi 8, na kwa mwaka huu wilaya ya Newala inaadhimisha kwa kufanya shughuli mbalimbali mdahalo, maonyesho ya wajasiriamali pamoja na usiku wa Mwanamke yakianzia tarehe 4 na kuhitimishwa tarehe 6.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa