Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Newala Bi. Shamim Mwariko amewataka wanawake kuchukua hatua za kuwalinda wajawazito ili kuondokana na changamoto ya vifo wakati wa kujifungua.
Ameyasema hayo Machi mosi 2023 katika viwanja vya Hospitali ya Mji Newala wakati anaongea na wanawake waliojitokeza kwenye ufunguzi wa wa maadhimisho ya juma la siku ya mwanamke duniani ngazi ya Halmashauri.
Mkurugenzi huyo amewaeleza wanawake hao kuwa Newala bado ina changamoto ya vifo vya wajawazito vinavyotokana na uelewa mdogo wa masuala ya lishe unaopelekea kuwa na damu pungufu wakati wa kujifungua jambo linalo ongeza hatari ya vifo kwa wazazi.
Aidhai Mwariko amewaomba wanawake hao kuwa mstari mbele katika kuishauri jamii katika kuzingatia afya ya Mama na mtoto na kuacha mazoea ya matumizi ya vitu visivyo na msaada kama ulaji wa udongo na mkaa.
Katika hatua nyingine amewahasa mabinti kuulinda usichana wao na kuacha kujirahisisha kwa kufanya hivyo wataongeza thamani yao na ya mwanamke katika jamii.
Katika siku hii ya ufunguzi wa maadhimisho haya wanawake wa Halmashauri ya Mji Newala wameadhimisha kwa kufanya maandano ya hamasa, kufanya usafi katika hospitali ya Mji Newala, kuwafariji wanawake waliojifungua, wajawazito walio wodini na watoto waliolazwa pamoja na kuwatembelea wanawake walio gereza la Newala.
Kilele cha Siku ya Mwanamke duniani katika Halmashauri ya Mji Newala kitafanyika Jumamosi Tarehe 04 Machi 2023 katika kijiji cha Namiyonga.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa