Watumishi ya Halmashauri ya mji Newala wamepata mafunzo ya matumizi ya mfumo wa PlanRep na FFARS kwa ajili ya maandalizi ya bajeti ya halmashauri kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Mafunzo hayo ya siku tatu yamefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo kuanzia Disemba 13-15, 2021 yakiwahusisha watumishi kutoka idara na vitengo mbalimbali vya halmashauri hiyo.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo mwezeshaji kutoka TAMISEMI Ndg. Frank Omollo amesema mafunzo hayo yamelenga kuwaogezea watumishi ujuzi utakaosaidia kurahisisha utumiaji sahihi wa mifumo na kutoa msaada wakati wa uandaaji bajeti.
Aidha Omollo ameeleza kuwa mafunzo hayo yanasaidia katika upangaji wa bajeti za idara na vitengo vya halamshauri kwa kuzingatia vipaumbele vya serikali katika sekta husika kwa kuanzia ukusanyaji mapato na matumizi yake pasipo kuathiri bajeti kuu.
Akiongea mara baada wa mafunzo hayo Afisa TEHAMA wa Halmashauri hiyo Bw. Daud Matandiko amesema, serikali inafanya jambo la muhimu kupeleka mafunzo wa watumishi wa ngazi zote hatua ambayo inasaidia kuwapunguzia kazi wakati wa ujazaji wa taarifa kwenye mpango wa uandaaji bajeti ukizingatia kwasasa mpango umeongeza bajeti kwenye ngazi ya Kata na Vijiji.
Baadhi ya watumishi waliopata mafunzo hayo wasema wamefurahishwa na mafunzo hayo kwa kuwa yatakuwa msaada kwao wa kufuata taratibu za kibajeti kutokana na vipaunbele vinavyohitajika pamoja na kupata uelewa wa matumizi ya mifumo ya elektroniki.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki milikiĀ©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa