Zoezi la kuchanja mifugo halmashauri ya Mji Newala linaendelea vizuri ambapo mpaka sasa Mbuzi na Kondoo 1556 wamepatiwa chanjo na sotoka pamoja na Ng’ombe 111 wameshapatiwa chanjo ya homa ya mapafu.
Mratibu wa zoezi hilo afisa ugani wa kata ya Nagwala anayeshughulikia mifugo Ndg. Rajabu Killo amesema kuna mwitikio nzuri wa wafugaji ambapo mpaka sasa wameshazifikia kata 8 kati ya 16 kutoa chanjo hiyo ya zuruku.
“Zoezi linaenda vizuri tulianza na Kondoo na Mbuzi kwa kata 8 za hapa mjini mpaka sasa tumechanja mbuzi 1556 na leo tumeanza Ng’ombe tumeshachanja ng’ombe 111 mpaka sasa hatunachangamoto yoyote.”
Aidha pia Killo amewaomba wananchi wafugaji waendelee kuwaunga mkono kwa kujitokeza kufanikisha utoaji wa chanjo hiyo ili waweze kufikia malengo yaliyowekwa na kuilinda mifugo yao na maradhi yanayoweza kuepukika.
Mmoja wa wafugaji kutoka mtaa wa Nangwala chini Bi. Rose Gadau ameishukuru serikali kwa kuwapunguzia mzigo wa kuhudumia mifugo kwa awali alikua anatumia shilingi 2000 kuchanja ng’ombe mmoja lakini ni shilingi 500 kwa ng’ombe mmoja.
Aidha amewashauri wafugaji wengine kutumia fursa hiyo kwa kuwa zipo hasara mifugo isipopata kinga huku akiiomba serikali kuendelea kuwakumbuka na kuleta chanjo hizo kwa wakati.
“nawaambia wenzangu wafugaji kuchanja sio kwamba tunapata hasara kuna faida, hii chanjo nimeifurahia tunaomba iwe inakuja kwa wakati, kwa sababu mwaka jana mimi nilikuwa na ng’ombe 10 lakini ulipoanza ugonjwa wote walikufa wakabakia hao wawili”.
Idara ya Kilimo, uvuvi na mifugo ya halmashauri ya Mji Newala kwa sasa inaendelea na zoezi la kitaifa la kutoa chanjo na utambuzi mifugo ya Ng’ombe, mbuzi na kondoo.
Newala-Mtwara
Anwani ya Posta: P.O.BOX 39
Simu: (+255) 023 2935398
Mobile: PS (0684439199)
Barua pepe: info@newalatc.go.tz
Haki miliki©2017 NTC. Masharti yote yanazingatiwa